Bush akamilisha ziara yake ya mashariki ya kati | Habari za Ulimwengu | DW | 17.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bush akamilisha ziara yake ya mashariki ya kati

CAIRO:

Rais George W.Bush amekamilisha ziara yake ya siku nane katika eneo la Mashariki ya kati kwa ziara fupi nchini Misri.

Mkutano wake na rais Hosni Mubarak wa Misri, uligubikwa na mgogoro wa Isreal na Palestina. Akizungumza katika hoteli ya Sharm el-Sheikh, rais Bush ameishukuru Misri kwa kuunga mkono mchakato wa amani na kuwa na matumaini kuwa suluhisho litapatikana.Aidha Bush ametoa matumaini kuwa Misri itapiga hatua u mbele zaidi kuelekea demokrasia kamili.Kipindi kilichopita Marekani imekuwa ikiikosoa Misri kuhusu suala la haki za binadamu na jinsi inavyoandama vyombo vya habari vinavyojitegemea. Pia Bush amesema kuwa Syria na Iran ni lazima zikomeshe kuingilia siasa za Lebanon na kuziomba nchi zingine katika kanda hiyo kumuunga mkono Waziri Mkuu Fouad Siniora wa Lebanon.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com