1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUNIA:Maiti zagunduliwa katika makaburi ya jumla

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpd

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamegundua makaburi makubwa matatu yaliokuwa na maiti za watu 30,ikidaiwa kuwa watu hao waliuawa na askarijeshi kwenye kambi ya kijeshi kaskazini-mashariki mwa Kongo. Mwendesha mashtaka wa kijeshi katika wilaya ya Ituri,John Penza amesema,maafisa wawili wa kijeshi wamekamatwa baada ya makaburi hayo kugunduliwa na afisa mmoja ameshakiri kuhusika na tukio hilo.Wanawake na watoto ni miongoni mwa maiti zilizogunduliwa kwenye kambi ya kijeshi baada ya mashahidi kuwashutumu wanajeshi kwa mauaji ya watu darzeni kadhaa miezi miwili iliyopita.Kambi hiyo ipo Bavi,kama kilomita 60 kusini mwa mji wa Bunia.