1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani latambua mauaji ya Wayazidi ya mwaka 2014

Tatu Karema
19 Januari 2023

Bunge la Ujerumani Bundestag, limeyatambua mauaji ya Wayazidi ya mwaka 2014 yaliyofanywa na wanajihadi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS kama mauaji ya halaiki na kutaka hatua zichukuliwe ili kuisaidia jamii hiyo

https://p.dw.com/p/4MRdn
Berlin Bundestag Kuppel
Picha: Michael Sohn/AP Photo/picture alliance

Katika hatua iliyopongezwa na wawakilishi wa jamii hiyo ya Wayazidi, wabunge katika bunge hilo wameupitisha muswada huo. Bunge hilo limesema limechukua hatua hiyo kufuatia tathmini ya kisheria iliyofanywa na Umoja wa Mataifa. Ujerumani inafuata nyayo za nchi nyengine kama Australia, Ubelgiji na Uholanzi kuyatambua mauaji hayo kama mauaji ya halaiki. Bunge la Ujerumani limesema uhaini uliofanywa na wanamgambo wa Dola la Kiislamu ulikuwa na lengo la kuiangamiza kabisa jamii ya Wayazidi.