BRUSSELS: Misaada ya kiutu iruhusiwe kwenye shida | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Misaada ya kiutu iruhusiwe kwenye shida

Umoja wa Ulaya una hofu kuwa mapigano yaliyozuka upya nchini Sri Lanka,yatahatarisha majadiliano ya amani yaliopangwa kufanywa kati ya serikali na waasi wa Tamil Tigers.Finland iliyoshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita,imetoa wito kwa pande zote mbili kuleta hali itakayosaidia majadiliano kufanywa kwa mafanikio. Majadiliano ya amani yamepangwa kufanywa mjini Geneva nchini Uswissi tarehe 28 na 29 mwezi huu.Serikali ya Sri Lanka na waasi wamehimizwa kuhakikisha kuwa misaada ya kiutu inaruhusiwa kupelekwa katika maeneo yalioathirika kwa mapigano.Vile vile wahakikishe usalama wa wafanyakazi wa mashirika yanayotoa misaada.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com