BERLIN:Waziri Steinmeier aanza ziara ya Latin Amerika
16 Aprili 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank- Walter Steinmeier yupo njiani kuelekea bara la Latin Amerika ambapo atafanya ziara ya siku tano.
Waziri Steinmeier pia anatarajiwa kukutana na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Ban Ki -Moon mjini New York kuzungumzia juu ya mgogoro wa Darfur.