BERLIN : Ujerumani yavunja rekodi ya biashara ya kigeni | Habari za Ulimwengu | DW | 09.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Ujerumani yavunja rekodi ya biashara ya kigeni

Kuongezeka kwa usafirishaji wa bidhaa nchi za nje kwa Ujerumani kwa mwaka 2006 kumeweka rekodi ya biashara ya kigeni ya ziada ya uero bilioni 162.

Usafirishaji huo wa bidhaa nchi za nje umeongezeka kwa asilimia 13 na kufikia euro bilioni 894 na hiyo kuifanya Ujerumani iendelee kushikilia dhima yake ya kuwa msafirishaji mkubwa duniani wa bidhaa nchi za nje kwa mwaka wa nne mfululizo.

Uagizaji wa bidhaa zinazoingia Ujerumani umefikia euro bilioni 713 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 kwa mwaka 2005.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com