Berlin. Ujerumani na Italia wakaribisha ripoti ya Barker. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Ujerumani na Italia wakaribisha ripoti ya Barker.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kiongozi mwenzake wa Italia Romano Prodi wameikaribisha ripoti hiyo kuhusu Iraq, hususan katika wito wa kuyahusisha mataifa jirani ya Iraq katika juhudi za kidiplomasia kuweza kupata suluhisho katika mzozo huo.

Hapo mapema mratibu wa serikali ya Ujerumani katika masuala ya uhusiano na Marekani, Karsten Voigt, amesema kuwa Ujerumani itakuwa tayari kusaidia ujenzi mpya nchini Iraq iwapo hali ya usalama itakuwapo.

Pia amesema kuwa Ujerumani na bara la Ulaya watakuwa tayari kuchukua jukumu la kidiplomasia lenye lengo la kupata uungwaji mkono wa Syria na Iran katika hatua za amani nchini Iraq.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com