BERLIN: Condoleezza Rice ahudhuria mkutano kuhusu Mashariki ya Kati mjini Berlin | Habari za Ulimwengu | DW | 21.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Condoleezza Rice ahudhuria mkutano kuhusu Mashariki ya Kati mjini Berlin

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, yumo mjini Berlin hapa Ujerumani kuhudhuria mkutano wa pande nne zinazoudhamini mpango wa amani ya Mashariki ya Kati.

Condoleezza Rice anatarajiwa kukutana hii leo na waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, na kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel.

Katika mkutano huo, Bi Rice atawaeleza viongozi hao wa Ujerumani juu ya mazungumzo yake na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas waliyokuwa nayo juzi Jumatatu mjini Jerusalem.

Mazungumzo hayo yalifeli kufikia makubaliano ya maana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com