Beirut. Vikosi vya mwisho vya Israel vyaanza kuondoka. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Beirut. Vikosi vya mwisho vya Israel vyaanza kuondoka.

Vikosi vya jeshi la Israel vilivyoko kusini mwa Lebanon vimeanza awamu ya mwisho ya kuondoka kutoka maeneo hayo chini ya masharti ya azimio la umoja wa mataifa ambalo limemaliza mapigano ya hivi karibuni baina yake na wanamgambo wa Hizboulah.

Waandishi wa habari wameona mabuldoza na vifaa vingine vya kiufundi vikisafirishwa kurejea nyumbani kwa barabara kwenda nchini Israel.

Maafisa wa ulinzi wa Israel wamesema kuwa wanamatumaini kuwa vikosi vya mwisho vya jeshi la nchi hiyo vitaweza kuondoka kabla ya siku kuu ya Yom Kippur, ambayo inaanza jioni ya Jumapili.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa mamia kadha ya wanajeshi pamoja na magari kadha ya deraya yamebaki nchini Lebanon.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com