Ban kupitia upya sera ya MONUC.
7 Oktoba 2010Matangazo
Ban Ki Moon amesema Umoja wa mataifa unapaswa kuwa wenye uhalisi, na amekiri kuwepo kwa idadi ndogo ya walinda amani hao, ambao wameelemewa na ukubwa wa nchi hiyo, pamoja na udogo wa rasilimali zao.
Kikosi hicho cha kulinda amani cha umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mara kadhaa kimekuwa kikikosolewa kwa kutokuwa na uwezo wa kuzuia visa vya ubakaji, matukio ambayo yalitokea kwa siku kadhaa julai mwaka huu na eneo ambalo liko kilomita 20 kutoka katika makao ya kikosi hicho.
Wiki hii, Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba kiongozi wa waasi wa MaiMai Cheka, kundi ambalo linadaiwa kufanya uhalifu huo wa ubakaji, Luteni kanali Mayele amekamatwa.