BAGHDAD:Mashambulio ya kujitolea muhanga yalenga wateja madukani | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Mashambulio ya kujitolea muhanga yalenga wateja madukani

Nchini Irak,watu wasiopungua 15 wameuawa na zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika miripuko mawili ya bomu iliyotokea,mashariki ya mji mkuu Baghdad. Mashambulio hayo ya kujitolea muhanga yalilenga barabara iliyojaa watu,katika eneo la biashara. Wakati huo huo vikosi vya Marekani vimesema kuwa vimewaua wanamgambo 14 katika mashambulio ya angani,karibu na Baghdad ambako wanamgambo wa madhehebu ya Sunni wanapigana na vikosi vya serikali ya Irak na vya Marekani.Hapo awali,jeshi la Marekani lilifichua kuwa 4 kati ya wale wanajeshi 5 wa Kimarekani waliouawa katika mji takatifu wa Washia Kerbala,walitekwa nyara na kuuliwa na watu waliovaa sare za kijeshi zilizofanana na zile za jeshi la Marekani.Maelezo ya shambulio hilo ambalo lilitokea tarehe 20 Januari,yalitolewa kwa mara ya kwanza baada ya spika mpya wa Baraza la wawakilishi la Marekani,Bi.Nancy Pelosi kufanya ziara ya ghafula nchini Irak.Pelosi ametoa mwito kwa serikali ya Irak,kuchukua dhima ya kimsingi kulinda usalama nchini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com