Baghdad.Idadi ya vifo yaongezeka na kuvunja rekodi huko nchini Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad.Idadi ya vifo yaongezeka na kuvunja rekodi huko nchini Iraq.

Vifo kutokana na mfululizo wa mabomu yakuripuliwa kwa gari vimeongezeka katika maeneo ya ngome ya Washia huko Sadr City mjini Baghdad.

Polisi nchini Iraq wamesema, hapo jana idadi hiyo ilifikia watu 202 na zaidi ya 250 wamejeruhiwa.

Aidha Madaktari wamesema, wengi wa watu waliojeruhiwa hali zao ni mbaya sana na ni bahati nasibu kwao kuweza kuishi.

Shambulio hili ni kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu mwezi March mwaka 2003 wakati majeshi yanayoongozwa na Marekani kuivamia Iraq.

Wakati huo huo Serikali ya Iraq imetangaza amri ya kutotoka nje ikihofia mashambulio ya kulipiza kisasi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com