BAGHDAD: Mashambulizi ya bomu yameua 14 Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 16.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mashambulizi ya bomu yameua 14 Irak

Si chini ya watu 14 wameuawa katika mashambulizi matatu ya bomu nchini Irak.Shambulizi lililosababisha idadi kubwa kabisa ya vifo, lilitokea katika mtaa mmoja wa Baghdad ambako Washia wengi huishi.Katika shambulio hilo watu 8 waliuawa baada ya mshambulizi aliejitolea muhanga kuligonga gari lake kwenye kituo cha jeshi cha ukaguzi.Kwa upande mwingine,maafisa wa majeshi ya Marekani wamethibitisha kuwa wanajeshi wake 4 waliuawa katika mripuko mwingine wa bomu uliotokea kando ya barabara,magharibi ya mji mkuu Baghdad.Wakati huo huo,ripoti mpya iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon inasema mashambulizi dhidi ya raia wa Kiiraki na vikosi vya muungano vinyvoongozwa na Marekani yamefikia kiwango cha juu kabisa katika kipindi kilichopindukia miaka mitatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com