BAGHDAD: Mapambano ya kimadhehebu yanaendelea Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mapambano ya kimadhehebu yanaendelea Irak

Mapambano kati ya makundi ya kimadhehebu yameendelea siku ya Ijumaa katika mji mkuu wa Irak Baghdad,kufuatia mashambulio ya bomu yaliyoua zaidi ya watu 250 siku ya Alkhamisi. Katika mashambulio hayo,mabomu yalipangwa kuripuka moja baada ya jingine.Miripuko hiyo hasa ilitokea katika mitaa yenye wakazi wengi wa Kishia.Siku ya Ijumaa katika kile kinachotazamwa kama ni mashambulio ya kulipiza kisasi,watu wenye bunduki walichoma moto si chini ya misikiti minne ya Wasunni na idadi fulani ya nyumba pia zilitiwa moto.Katika mashambulio hayo,hadi watu 25 waliuawa.Wanamgambo wengine waliwateka nyara Wasunni 6 waliokuwa wakitoka msikitini baada ya sala ya Ijumaa na wakamwagiwa mafuta ya taa na kutiwa moto.Wakati huo huo wafuasi wa Moqtada al-Sadr,kiongozi wa kidini wa Kishia,alie na itikadi kali,wametishia kujitoa serikalini na bungeni, ikiwa waziri mkuu Nuri al-Maliki atakutana na rais George W.Bush wa Marekani juma lijalo nchini Jordan.Ikulu ya Marekani imesema mkutano huo utafanywa kama ilivyopangwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com