1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba mtakatifu kuongoza misa ya pasaka leo

Charo, Josephat23 Machi 2008

Papa Benedict XVI anatarajiwa kuwabariki waumini

https://p.dw.com/p/DT2S
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Baba mtakatifu Benedict XVIPicha: AP

Kiongozi wa kanisa Katoliki papa Benedict XVI anatarajwia hii leo kuongoza misa ya hadhara ya pasaka katika uwanja wa St Peter´s. Misa hiyo itakayoandamana na baraka ya pasaka itaanza saa tatu unusu na itaonyeshwa moja kwa moja katika nchi 57 duniani.

Hapo jana baba mtakatifu Benedict XVI aliwabatiza waumini saba wakatoliki, akiwemo muamini wa zamani wa dini ya kiislamu, katika misa iliyofanyika katika uwanja wa St Peters Basilica. Magdi Allam, mwenye umri wa miaka 55 ni mwandishi wa habari mtaliani mwenye nasaba ya Misri, alikuwa musilamu wa msimamo wa wastani kabla kuamua kuwa muami wa dini ya kikatoliki.

Misa ya Jumamosi usiku inaashiria wakati Yesu Kristo alipofufuka kutoka kwa wafu na kitamaduni huadhimishwa kwa ubatizo wa watu wazima.