ATHENS: Ndege ya abiria ya Ugiriki yatua ghafla nchini Ireland | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ATHENS: Ndege ya abiria ya Ugiriki yatua ghafla nchini Ireland

Ndege ya abiria ya Ugiriki iliyokuwa njiani kwenda mjini New York Marekani imelazimika kutua ghafla katika uwanja wa ndege wa Shannon magharibi mwa Ireland leo alfajiri.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya watu wasiojulikana kupiga simu na kusema mlikuwa na bomu la Saddan Hussein ndani ya ndege hiyo. Watu hao waliozungumza kama warabu, walitoa onyo lao kwa lugha ya kiingereza.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Olypmpic Airlines, ilikuwa imeondoka mjini Athens Ugiriki ikiwa imewabeba abiria 183 na wafanyakazi 12.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com