1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA : Watu 20 wafariki katika ajali ya basi

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBom

Watu 20 wameuwawa baada ya basi dogo na lori lenye kubeba mchanga kugongana huko Arusha mji ulioko kaskazini mwa Tanzania.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Basilio Matei amesema leo hii watu wote waliokufa walikuwemo kwenye basi hilo dogo wakati lori hilo lilipokuwa likijaribu kulipita gari jengine kuligonga basi hilo.Watu 19 walifariki papo hapo na mmoja alikufa baadae.

Ajali hiyo iliotokea jana inakuja katika kipindi kisichozidi wiki moja baada ya basi kupinduka katika mkoa wa Singida kaskazini magharibi mwa Tanzania kuunguwa moto na kuuwa watu 16.