ANCIENT OLYMPIA:Idadi ya wakiouwawa kwenye moto yafika watu 60 | Habari za Ulimwengu | DW | 27.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANCIENT OLYMPIA:Idadi ya wakiouwawa kwenye moto yafika watu 60

Idadi ya watu waliouwawa katika ajali ya moto huko Ugiriki imefikia watu 60.

Moto huo wa porini uliochukua muda wa siku tatu sasa umesababisha madhara makubwa katika maeneo mengi nchini humo na kuzusha hali ya wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakaazi.

Hata hivyo Wafanyikazi wa kupambana na mioto wakisaidiwa na ndege wameweza kuzuia moto huo kuharibu eneo kuliko asisiwa mashindano ya Olimpiki.Mioto ya porini nchini Ugiriki imesababisha kuharibiwa kwa vijiji misitu pamoja na mashamba katika muda wa siku tatu na kuifanya serikali siku ya jumamosi kutangaza hali ya hatari.

Kwa mujibu wa msemaji wa kitengo kinachohusika na majanga ya mioto karibu nusu nzima ya nchi imeteketezwa.

Wananchi wengi wameomba msaada wa zima moto kupitia televisheni lakini tayari kitengo cha zima moto kimezidiwa nguvu na wananchi wengi sasa wanailaumu serikali kwa kutowasaidia.

Serikali kwa upande mwingine inalaumu kwamba moto huo umesababishwa na watu kimakusudi na imetoa zawadi ya kitita cha fedha kwa mtu atakayetoa habari zitakazosaidia kukamatwa watu hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com