ADDIS ABABA : 74 wauwawa katika machimbo ya mafuta | Habari za Ulimwengu | DW | 25.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA : 74 wauwawa katika machimbo ya mafuta

Takriban wafanyakazi 74 wameuwawa katika shambulio la watu wenye silaha kwenye machimbo ya mafuta yanayosimamiwa na China mashariki ya Ethiopia.

Shirika la habari la serikali nchini China Xinhua limesema kwamba watu tisa miongoni mwa waliouwawa ni Wachina na 65 waliobakia ni raia wa Ethiopia.Watu hao wenye silaha pia wamewateka nyara wafanyakazi saba wa Kichina kutoka machimbo hayo ya mafuta kwenye jimbo lenye mzozo la Ogaden ambalo linapakana na Somalia.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini baadhi ya maafisa wanatuhumu yumkini likawa ni kundi la waasi la Ukombozi wa Taifa la Ogaden.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com