ACCRA: Waghana waadimisha miaka 50 ya uhuru | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ACCRA: Waghana waadimisha miaka 50 ya uhuru

Waghana wamejitokeza kwa wingi hii leo kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru kutoka kwa Uingereza. Rais wa Ghana, John Kufuor, amesema uhuru wa Ghana ni sababu ya Afrika nzima kusherehekea.

Maelfu ya Waghana wamekusanyika katika uwanja wa uhuru mjini Accra, mahali ambapo kunafanyika magwaride ja kijeshi. Eneo hilo ni karibu na kiwanja cha Old Polo ambako Kwame Nkurumah, rais wa kwanza wa Ghana, alisherehekea uhuru kama waziri mkuu.

Uhuru wa Ghana uliyafungulia mlango mataifa mengine barani Afrika kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com