1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yellen: Uhusiano wa China na Marekani una mwelekeo sahihi

9 Julai 2023

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amesema, uhusiano kati ya Marekani na China umepiga hatua na uko katika mwelekeo sahihi.

https://p.dw.com/p/4TdIg
China Peking | Finanzministerin der USA Janet Yellen in China
Picha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Yellen ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, wakati ziara yake ya siku nne nchini humo ikielekea ukingoni.

Amesema siku mbili za mazungumzo kati ya mataifa hayo mawili zimekuwa zenye manufaa ingawa yako masuala ambayo hawakubaliani.

Soma zaidi: Yellen aikosoa China kwa hatua kali dhidi ya kampuni za Marekani

Kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la habari la China Xinhua, serikali ya nchi hiyo imeyaelezea mazungumzo kati ya Yellen na makamu wa waziri mkuu mwenye dhamana ya kusimamia sera za uchumi nchini humo He Lifeng kuwa ya manufaa, ya wazi na ya kina.

Hata hivyo China imeonesha wasiwasi wake kuhusu vikwazo ilivyowekewa na Marekani. Kwenye ziara hiyo, Waziri wa fedha wa Marekani alikutana pia na kufanya mazungumzo na waziri mkuu Li Qiang.