1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wazanzibari wahimizwa kudumisha amani

Salma Said28 Aprili 2021

Wazanzibari wametakiwa kuendeleza amani iliyopo baada ya uchaguzi licha ya changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa 2020 ambao ulifuatiwa kwa kurejeshwa tena mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa.

https://p.dw.com/p/3sglM
Tansania | Zanzibar Revolution Day
Picha: Salma Said/DW

Taasisi ya Friends of Zanzibar kwa kushirikiana na ofisi ya Mufti ndio inayoandaa mikutano katika wilaya zote 11 za Unguja na Pemba na kukutana na viongozi wa ngazi tofauti wakiwemo Masheha, Maimamu wa Misikiti, walimu wa Madrassa na wananchi mbali mbali lengo likiwa kuteremsha ujenzi wa amani katika ngazi za chini za kijamii.

Soma pia: 

Matumaini ya Wazanzibari katika urais wa Samia Suluhu Hassan

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Kaabi amesema katika kipindi kilichopita Maridhiano yalitetereka na hivyo kuna kila sababu ya suala la amani kuendelezwa ili wananchi waishi katika hali ya amani ya kudumu ili yale ambayo yalitokea nyuma yasijirudie.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi Regina Heiss amesisitiza ujenzi wa amani kuwa endelevu na kuahidi serikali yake kuendelea kuisadia Zanzibar katika ujenzi wa demokrasia na amani.

Wito umetolewa kwa Wazanzibari kujenga utamaduni wa kuvumiliana.
Wito umetolewa kwa Wazanzibari kujenga utamaduni wa kuvumiliana.Picha: DW/S. Said

Katibu wa Taasisi ya Amani Sheikh Abubakar Kabudi amewasisitiza wazanzibari kuishi kwa upendo na kujenga utamaduni wa kuvumiliana.

Soma pia: Rais Mwinyi ashauri kubadilishwa mfumo wa uendeshaji wa mashirika

Nao baadhi ya masheha na washiriki wa mkutano huo wamewahimiza wanasiasa kujizuwia kufanya ushawishi wa uvunjifu wa amani kwani kila nyakati za uchaguzi mambo hayo hujirejea.

Mikutano hiyo ni muendelezo wa mkutano mkubwa wa kitaifa uliofanyika Januari mwaka huu unaozungumzia umuhimu wa amani na kuwashirikisha mabalozi mbali mbali na wanachama wa nchi za mashariki mwa Afrika zikiwemo Msumbiji, Malawi, DR Congo, Rwanda, Uganda, Burundi, Kenya, Tanzania na mwenyeji Zanzibar ukiwa na lengo la kuwaeleza wazanzibari umuhimu wa kukaa pamoja na kusonga mbele kimaendeleo.