1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu wawili wauawa kwenye shambulio la droni Kherson

Saleh Mwanamilongo
2 Mei 2026

Katika pwani ya Bahari Nyeusi ya Ukraine, shambulio la Urusi liliharibu miundombinu ya bandari katika mji wa Odesa. Hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa.

https://p.dw.com/p/5DA8j
Urusi, Mkoa wa Kherson 2026 | Uharibifu baada ya shambulio la droni la Ukraine huko Khorly
Moto uliozuka Ijumaa kufuatia shambulio la Ukraine kwenye kituo cha mafuta katika mji wa Tuapse uliopo kwenye Bahari Nyeusi ulizimwa JumamosiPicha: Daniil Mikhailov/TASS/ZUMA/picture alliance

Watu wawili, mwanaume na mwanamke, wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa katika shambulio la droni la Urusi lililolenga basi dogo katika mji wa Kherson kusini mwa Ukraine. Gavana wa kijeshi wa eneo hilo, Oleksandr Prokudin, amesema waliojeruhiwa, wakiwemo wanaume sita na mwanamke mmoja, wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Mji wa Kherson ulitekwa na majeshi ya Urusi mwanzoni mwa uvamizi mkubwa wa mwaka 2022, lakini baadaye walijiondoa kufuatia mashambulizi ya kujibu ya Ukraine.

Tangu wakati huo, eneo la mapigano limekuwa karibu na mji huo, ambao unaendelea kushambuliwa mara kwa mara kwa droni na makombora ya masafa marefu kutoka Urusi.