1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUhispania

Uhispania yaitaka Israel kumuachilia raia wake aliyekamatwa

2 Mei 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania, José Manuel Albares, ameitaka Israel kumuachie huru raia wa Uhispania aliyekamatwa baada ya jeshi la majini la Israel kuzuia msafara wa misaada kuelekea Gaza.

https://p.dw.com/p/5DAOW
Hispania | Barcelona 2026 – Msafara wa misaada kwa Gaza wa “Global Sumud Flotilla” katika bandari
Uhipsania yaitaka Israel kumuachia huru raia wa Uhispania aliyekamatwa baada ya jeshi la majini la Israel kuzuia msafara wa misaada kuelekea GazaPicha: Joan Mateu Parra/AP Photo/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania, José Manuel Albares, ameitaka Israel kumuachie huru raia wa Uhispania aliyekamatwa baada ya jeshi la majini la Israel kuzuia msafara wa misaada kuelekea Gaza. Amesema kukamatwa huko kulifanyika katika maji ya kimataifa nje ya mamlaka ya Israel, na kukiita kitendo kisicho halali.

Israel inamshutumu raia huyo, Saif Abukeshek, kuwa na uhusiano na kundi la Hamas, madai ambayo Uhispania inasema hayajathibitishwa. Abukeshek pamoja na mwanaharakati wa Brazil wamepelekwa Israel kwa kuhojiwa.

Tukio hilo linajiri baada ya jeshi la Israel kuzuia meli zaidi ya 20 za misaada karibu na kisiwa cha Krete. Waandaaji wa msafara huo wanasema wataendelea na safari yao ya kuelekea Ukanda wa Gaza mara hali ya hewa itakapotulia.