1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wa boti ya msaada ya Flotilla wawasili Ugiriki

1 Mei 2026

Wanaharakati waliokuwa kwenye msafara wa boti ya msaada ya flotilla iliyokuwa ikielekea Gaza ambayo ilikamatwa na wanajeshi wa Israel karibu na kisiwa cha Crete nchini Ugiriki, wamewasili leo katika kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/5D7UR
Itali Sicily 2026 | Global Sumud Flotilla
Wanaharakati wapakia bidhaa za misaada kwa boti za msaada za flotilla tayari kuanza safari kuelekea Gaza kutoka Italia mnamo Aprili 25, 2026Picha: Baris Seckin/Anadolu Agency/IMAGO

Wakisindikizwa na walinzi wa pwani ya Ugiriki, wanaharakati hao wapatao 175 walisafirishwa kwa mabasi manne hadi mji ambao jina lake halikutajwa jina na mamlaka.

Awali, wizara ya mambo ya nje ya Israel ilisema takriban wanaharakati 175 walikuwa wametolewa kwenye boti zaidi ya 20 jana Alhamisi. Waandaaji wa safari hiyo walitaja idadi hiyo kuwa 211.

Katika ujumbe aliotuma jana jioni kwenye mtandao wa X, waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar, aliishukuru Ugiriki kwa kukubali kuwapokea wanaharakati hao.

Serikali kadhaa za Ulaya zenye raia miongoni mwa waliokamatwa, zimeitaka Israel kuwaachilia huru wanaharakati hao na kuitaja hatua yake hiyo kuwa ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.