Watu 16 wauwawa kwenye mapigano ya siku mbili Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu 16 wauwawa kwenye mapigano ya siku mbili Mogadishu

-

MOGADISHU

Watu wanane wameuwawa hii leo katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu kufuatia mapigano ya siku mbili yaliyoanza hapo jana.Kwa jumla watu 16 wameuwawa kutokana na mapigano hayo.Mji huo ulikuwa na utulivu wa kiasi wiki hii wakati wa mazungumzo ya amani yaliyosimamiwa na Umoja wa mataifa nchini Djibouti kati ya serikali ya mpito na viongozi wa upinzani wanaoishi nchini Eretrea.

Watu watano wakiwemo wanajeshi wawili wa serikali ya mpito waliuwawa katika mapigano ya usiku kaskazini mwa mji wa Mogadishu.Aidha wanajeshi wa Ethiopia wamewaua wanafunzi watatu waliokuwa wamevalia sare za shule lakini hawakuwa wamebeba vitabu hali ambayo iliwafanya kuwashuku kuwa ni wapiganaji.

Mazungumzo ya wiki hii ya kujaribu kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa Somalia hayakufanikiwa kupiga hatua kubwa baada ya maafisa wa upinzani kudai wanajeshi wa Ethiopia kwanza waondoke kwenye ardhi ya Somalia kabla ya kufanyika mazungumzo ya ana kwa ana.Wakti huohuo kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu imeonya kwamba hakuna dalili ya kuimarika hali ya mzozo wa kibinadamu ambayo wafanyikazi wa misaada wanasema huenda ikasababisha balaa kubwa kuwahi kushuhudiwa barani Afrika.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com