WASHINGTON:kituo cha kijeshi cha Marekani kwa Afrika kuwekwa Ujerumani kwanza | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:kituo cha kijeshi cha Marekani kwa Afrika kuwekwa Ujerumani kwanza

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani

Wizara ya ulinzi ya Marekani imeandaa mipango ya kujenga kitengo maalumu cha kijeshi kitakachoshughulikia bara la Afrika.

Marekani inapanga kwanza, kukiweka kitengo hicho katika mji wa Stuttgart kusini mwa Ujerumani kabla ya kukihamishia Afrika katika siku za usoni.

Kiasi cha dola milioni 50 kimetengwa kwa ajli ya mradi huo.

Rais G. Bush amesema kituo hicho kipya kitaimarisha ushirikiano baina ya Marekani na nchi za Afrika hasa katika harakati za kupambana na ugaidi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com