WASHINGTON: Mkutano juu ya kitisho cha ugaidi wa kinyuklia wiki ijayo nchini Morokko | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Mkutano juu ya kitisho cha ugaidi wa kinyuklia wiki ijayo nchini Morokko

Wajumbe kutoka nchi kiasi ya 10 watakutana mjini Rabat nchini Morokko kuzungumzia juhudi za kupambana na kile walichokitaja kitisho cha ugaidi wa kinyuklia: Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani inasema mkutano huo ni katika mpango ulioanzishwa na Marekani na Rushia mwezi Julai mwaka huu. Mkutano huo utawajumuisha wajumbe kutoka Marekani, Rushia, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italy, Japan, Canada, Uchina, Kazakhstan na Uturuki. Morokko, mwenyeji wa mkutano huo, inazingatiwa na Marekani pamoja na Rushia kuwa inachangia vya kutosha katika juhudi za kupambana na ugaidi duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com