1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasaudi wazidi kushinikizwa juu ya kutoweka kwa Khashoggi

Zainab Aziz
11 Oktoba 2018

Marekani imeongeza shinikizo kwa Saudi Arabia kutokana na kutoweka kwa mwandishi habari Jamal Khashoggi. Mkasa huo umesababisha wajumbe wa Marekani kutaka viongozi wa Saudi Arabia wachunguzwe.

https://p.dw.com/p/36LZ4
USA Präsident Trump spricht vor Anhängern über die Berufung von Kavanaugh an den Obersten Gerichtshof
Picha: Reuters/Y. Gripas

Rais wa Marekani Donald Trump ameelezea kutoridhishwa kwake na mkasa huo wa Kashoggi na ametishia kwamba nchi yake itasitisha mauzo ya silaha kwa Saudia kuhusiana na kutoweka kwa mwandishi habari huyo. Maneno ya Trump,yanalingana na ya seneta wa chama cha Republican Bob Corker anayezidi kuilaumu Saudi Arabia mshirika wa muda mrefu wa Marekani katika masuala ya usalama katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Mwandishi habari Jamal Kashoggi aliyetoweka
Mwandishi habari Jamal Kashoggi aliyetowekaPicha: Getty Images/AFP/M. Al-Shaikh

Bob Corker ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya nje ya baraza la seneti la Marekani ameelezea wasiwasi kuhusu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari Jamal Khashoggi. Amesisitiza kwamba kwa sasa uchunguzi kuhusu kilichotokea kwa Khashoggi, uelekezwe kwa Saudi Arabia.

Maafisa wa Uturuki wanaamini kuwa mwandishi habari Khashoggi aliyekuwa analiandikia gazeti la Marekani la Washington Post aliuliwa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul alipoutembelra aubalozi huo tarehe 2 mwezi huu wa Oktoba ijapokuwa hakuna ushahidi uliotolewa. Saudi Arabia imezikanusha tuhuma hizo ingawa pia haijatoa ushahidi wowote kuelezea vipi  Khashoggi alitoka kwenye ubalozi huo vipi alivyotoweka wakati ambapo mchumba wake alikuwa anamsubiri nje. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan pia ameongeza shinikizo lake kwa Saudi Arabia kutokana na kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari Jamal Khashoggi.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony BlairPicha: Reuters/K. Navntoft

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair amesema kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari Jamal Khashoggi ni masa wa kutisha sana unaokinzana na jitihada za mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohamed bin Salman za kuleta mabadiliko nchini mwake. Blair aliwaambia waandishi wa habari wa shirika la Reuters mjini London kwamba serikali za Marekani na Uingereza zimeeleza wazi kuwa ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike.

Mwandishi: Zainab Aziz/AP/RTRE/p.dw.com/p/36KJf

Mhariri: Saumu Yusuf