Wapalestina 41 wauawa Gaza | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wapalestina 41 wauawa Gaza

Wanajeshi wa Israel wamewaua Wapalestina 41 karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza

Wanajeshi wa Israel wamewaua Wapalestina 41 karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza wakati waandamanaji wenye ghadhabu wakiandamana kupinga hatua ya Marekani kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem. Hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa Afya.

Idadi hiyo ya vifo vya Wapalestina ndiyo ya juu zaidi kutokea kwa siku moja tangu kuanza kwa maandamano hayo Machi 30, na pia juu zaidi tangu vita vya Gaza vya 2014.

Maafisa wa afya wamesema kuwa Wapalestina 900 wamejeruhiwa, 450 wakiwa na majeraha ya risasi.

Mwandishi: John Juma/RTRE

Mhariri: Iddi Sessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com