1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Wanadiplomasia wa China na Marekani wafanya mazungumzo

Saumu Mwasimba
6 Juni 2023

Wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Marekani na China wamefanya mazungumzo yaliyoelezwa kuwa ya ufanisi huko Beijing na nchi zote mbili zimekubaliana kuacha wazi dirisha la mazungumzo ili kuepuesha mivutano.

https://p.dw.com/p/4SFzv
China | Daniel Kritenbrink Peking
waziri msaidizi wa mambo ya kigeni wa Marekani anayehusika na masuala ya Asia ya Kati na nchi za eneo la bahari ya Pasifik Daniel KritenbrinkPicha: Thomas Peter/REUTERS

Mikutano iliyofanyika kati ya maafisa wa China na Marekani wiki hii imefanikiwa kukifikia kile ambacho pande zoze mbili imekiita ufanisi,huku nchi zote zikikubali kuendeleza mawasiliano hata pale ambapo utawala wa Beijing unaonekana kubakia kwenye mwelekeo zaidi wa uchokozi kwa hatua za Marekani na kuacha wazi uwezekano wa kuendelea kuwepo kitisho cha kutokea vita vya wazi.

Tamko kutoka Washington na Beijing kuhusu mikutano iliyofanyika kati ya waziri msaidizi wa mambo ya kigeni wa Marekani anayehusika na masuala ya Asia ya Kati na nchi za eneo la bahari ya Pasifik Daniel Kritenbrink na maafisa wa China akiwemo naibu waziri wa mambo ya nje  Ma Zhaoxu,limesema yalikuwa ni mazungumzo yenye ufanisi.

Ingawa lazima tukumbushe kwamba siku ya Jumapili kabla hata ya kuwasili Kritenbrink mjini Beijing,jeshi la wanamaji la Marekani liliripoti kuhusu kile ilichokiita 'vitendo visivyokuwa salama'' siku ya Jumamosi baada ya meli za kivita za China kupita mbele ya  meli ya kufanya mashambulio ya Marekani katika eneo tete la ujia wa bahari la Taiwan,hatua iliyoizusha mtazamo wa kuwepo uwezekano wa kutokea makabiliano huko baadae ambayo huenda yakashindwa kudhibitiwa.

China | Daniel Kritenbrink und Sarah Beran | Besuch in Peking
Picha: https://www.fmprc.gov.cn

Na juu ya hilo ziara hii ya Kritenbrink pia ilikuja kimsingi baada ya China kuipuuza Marekani wiki iliyopita kwa kukataa kumualika waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Lloyd Austin ambaye alitaka kuwa na mkutano rasmi na mwenzake wa China lakini akakataliwa kweupe.

Lakini mazungumzo yaliyofanyika wiki hii yanaonesha kusifiwa na pande zote mbili taarifa iliyotoka wizara ya mambo ya kigeni ya China imesema pande zote mbili zilifanya mazungo ya ufanisi,na yaliyozaa matunda katika suala la kuunga mkono hatua ya kuimarisha mahusiano, kusimamia kwa usahihi na kuzidhibiti tofauti zilizopo.Marekani yasema mazungumzo na china ni muhimu ili kuepuka Mzozo

Marekani nayo kupitia wizara yake ya mambo ya nje ikatowa tamko Jumatatu usiku ikisema pande zote mbili zimezungumza kwa namna ambayo yalikuwa ni matungumzo yenye tija kama sehemu ya juhudi zinazoendelea kuimarisha na kuendelea na  mawasiliano baina ya nchi hizo mbili. Lakini pia kuendeleza juhudi za kidiplomasia katika ngazi za juu.

Utawala wa Marekani wa rais Joe Biden umeamua kutia msukumo kuimarisha mawasiliano na China katika wakati ambapo uhusiano  wa nchi hizo mbili zenye uchumi imara duniani umekuwa mbaya sana kutokana na masuala mbali mbali kuanzia Taiwan,ambayo China inadai ni milki yake mpaka shughuli za kijeshi katika eneo la Kusini la bahari ya China. Hata hivyo wakosoaji wamezitilia shaka  juhudi za Marekani kuelekea China wakitoa hoja kwamba, miongo kadhaa ya kuwepo juhudi hizo imeshindikana kuifanya China kubadili tabia yake.

Meli, China, Pasifiki, mzozo wa Taiwan
Ndege ya kivita ya China katika bahari ya Pacific karibu na TaiwanPicha: Japan's Ministry of Defense/AFP

Gazeti moja linaloegemea upande wa serikali ya China,la Global Times limeandika katika makala yake iliyochapishwa, Jumatatu usiku kwamba  mazungumzo ya hivi karibuni kati ya China na Marekani yameonesha pande zote zinajaribu kushughulikia mivutano japokuwa kitisho cha kutokea vita  bado kitaendelea kuongezeka ikiwa Washington haitoachana na  uchokozi wake na ikiwa pia haitokuwa mkweli katika kutaka kuimarisha mahusiano.China: Tuko tayari kusambaratisha hatua zozote za kuipatia Taiwan uhuru

Gazeti hilo limekwenda mbali zaidi kwa kusema mahusiano ya China na Marekani yameingia katika kile ilichokiita awamu''ngumu zaidi'' huku China ikiwa tayari kuweka uthabiti kwenye mahusiano hayo na kuwa tayari kwa uwezekano wa kuwa na ushirikiano,lakini pia itakuwa tayari kupambana kwa nguvu zote dhidi ya uchukozi wa Marekani.

Jana Jumanne waziri msaidizi wa Marekani,Kritenbrink,pale alipoulizwa na  waandishi habari mjini Beijing kuhusu hali ya uhusiano wake na China ilivyo kwa sasa, alisema wanafanya juhudi kubwa kuurekebisha uhusiano kadri wanavyoweza.

Cha kujikumbusha katika suala hili la mahusiano ya Marekani na China ni kwamba mnamo mwezi Februari mahusiano yalichukua mkondo mbaya zaidi kufikia mpaka waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kuifuta ziara yake ya kwenda China baada ya kuonekana kile Washington ilichosema ni Puto la ujasusi la China kuruka kwenye anga ya Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Kundi la wahamiaji wakiwasili katika eneo la Dover, Kent nchini Uingereza
Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW
Nenda ukurasa wa mwanzo