1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa nchi tatu za Ulaya kukutana na Zelensky

8 Desemba 2025

Viongozi wa nchi tatu za Ulaya wanakutana Jumatatu mjini London na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ili kuujadili mpango wa amani uliopendekezwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/54uxB
London I Viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Ukraine wakijadili kuhusu vita vya Ukraine
Kutoka kushoto: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: JUSTIN TALLIS/AFP

Rais Zelensky atakutana kwa mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na watajadili namna ya kujibu mapendekezo ya Marekani ya kukomesha vita kati ya Ukraine na Urusi.

Mazungumzo hayo  yatafanyika baada ya maafisa wa Ukraine kukamilisha mazungumzo ya siku tatu na wenzao wa Marekani kuhusu pendekezo hilo huku Ikulu ya White House ikiishinikiza Kiev kuuafiki mpango huo wa amani.

Hayo yakiarifiwa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amesema Ukraine haipaswi kulazimishwa kuachia ardhi yake kama sehemu ya makubaliano ya amani.