Mchezo wa ndondi ni mojawapo wa michezo maarufu ulimwengu japo washiriki wake ambao ni mabondia sio wengi vile ukilinganisha na michezo mengine. Miongoni mwa vijana, mchezo huu wa ndondi ambao ni mabondia wawili kupigana kwa kutumia ngumi pekee haujapokelewa kwa shangwe kubwa kama vile kandanda licha ya vijana wengi kuonekana kufanya mazoezi ya kutanua vifua na mikono.