SiasaUkraine
Utoaji umeme kwa mgao wawaathiri mamilioni ya Waukraine
10 Novemba 2025
Matangazo
Hali hiyo imejiri baada ya Urusi kushambulia miundo mbinu ya nishati mwishoni mwa wiki.
Kampuni ya taifa ya umeme nchini Ukraine Ukrenergo, imetangaza Jumatatu kuwa kutakuwa na mgao wa umeme wa saa kadhaa katika maeneo mbalimbali, kutokana na mzozo wa Urusi na Ukraine ambapo vikosi vya Urusi, vilishambulia vituo vya nishati kuelekea majira ya baridi kali.
Katika tukio jingine, shirika la Ukraine la kupambana na ufisadi limesema linafanya operesheni kubwa ya kufichua ufisadi katika sekta ya nishati ya nchi hiyo.
Shirika hilo limesema wamerekodi matukio makubwa ya uhalifu na kwamba uchunguzi huo ulishirikisha saa 1,000 za sauti zilizorekodiwa kwa kipindi cha miezi 15.