Migogoro
Urusi yazidungua droni 235 za Ukraine
14 Desemba 2025
Matangazo
Gavana wa Mkoa wa Volgograd amesema ghala la mafuta katika eneo lake liliwaka moto baada ya mabaki ya droni moja iliyodunguliwa kuanguka na kusababisha mlipuko.
Safari za ndege zasitishwa kwa muda
Mamlaka ya udhibiti wa anga nchini humo imesema pia takriban viwanja kumi vya ndege vikiwemo vya Moscow na Saint Petersburg vilitangaza kusitisha safari kwa muda usiku.
Hayo yanaendelea wakati ambapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuwa atahudhuria mazungumzo mjini Berlin yanayolenga kuvimaliza vita nchini mwake. Mjumbe Maalum wa Marekani Steve Witkoff anatarajiwa kuhudhuria majadiliano hayo lakini Urusi haitakuwa na muwakilishi.