1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: yapiga kura kushinikiza kusitishwa mapigano Gaza

Zainab Aziz
25 Machi 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajiandaa kupigia kura azimio la kushinikiza usitishwaji mapigano katika Ukanda wa Gaza ili kuruhusu kufikishwa misaada kwa Waislamu katika kipindi hiki cha Ramadhan.

https://p.dw.com/p/4e6DJ
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa latarajiwa kupiga kura ya kusitishwa mapigano GazaPicha: Angela Weiss/AFP/Getty Images

Kura hiyo itapigwa baada ya siku ya Ijumaa Urusi na China kutumia kura zao za turufu kupinga azimio lililoandaliwa na Marekani kuhusu kusitishwa mapigano kwenye mzozo kati ya Israel na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Marekani imetahadharisha kwamba kura itakayopigwa inaweza kuathiri makubaliano ya kumaliza mvutano yaliyoratibiwa na taifa hilo pamoja na Misri na Qatar, hali inayoibua wasiwasi wa kura nyingine ya turufu kutumiwa na Marekani.

Israel yazingira hospitali mbili zaidi zilizoko mji wa Khan Younis

Azimio hilo, lililowasilishwa na wajumbe 10 wa kuchaguliwa wa Baraza la Usalama linaungwa mkono na Urusi na China na mataifa 22 ya Kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa.