#UjerumaniYaamua - Watu wanaochukuliwa kama mifano na wagombea wakuu
Wanasiasa wenye mvuto wanaweza kutumika kama mifano, lakini pia wana mashujaa wao. Kutoka washindi wa Nobeli hadi wanadiplomasia wa Ufaransa, DW inaangazia watu hao ambao ni vigezo vya wagombea sita wakuu wa Ujerumani.
Angela Merkel (CDU): Marie Curie
"Marie Curie alikuwa ni mfano mkubwa kwangu nikiwa mdogo. Kulikuwa na watu wanne tu waliopata tuzo zaidi ya moja ya Nobeli, na alikuwa mwanamke pekee“ Anasema Kansela Angela Merkel. Kazi ya Marie Curie ya utafiti wa mionzi ilimpa tuzo ya Nobel ya masuala ya Fizikia mwaka 1903. Ugunduzi wake wa elementi za radium and polonium, ulimpatia kwa mara nyingine tuzo ya Nobel ya Kemia, mwaka 1911.
Martin Schulz (SPD): Willy Brandt
"Willy Brandt […] ni mtu wa mfano na mhamasishaji wangu. Maono yake kuhusu jamii haki katika Ulaya iliyoungana bado yananivutia sana hadi leo” anasema Schulz, pichani na sanamu ya Brandt. Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha Social Democrats na kansela wa Ujerumani ya Magharibi kati ya mwaka 1969 hadi 1974 anakumbukwa kama mhimili wa upatanisho kati ya Ujerumani Mashariki na Magharibi.
Cem Özdemir (Alliance '90/The Greens): Willy Brandt
"Willy Brandt alituonyesha kwamba siasa inahitaji maono, na inatakiwa kuwa zaidi ya utashi," anasema Özdemir. Akiwa mmoja wa wagombea wawili wa chama cha Kijani (pamoja na Katrin Göring-Eckardt), Özdemir anayaona mawazo mapana ya ya Brandt, pamoja na msukumo wa amani Barani Ulaya kama mwongozo. Picha hii ya Brandt akionekana amepiga magoti kwenye mnara wa mashujaa mjini Warsaw ni ya kihistoria.
Sahra Wagenknecht (The Left Party): Rosa Luxemburg
"Rosa Luxemburg “alikuwa mtu wa mfano kwangu. Ni mwanamke jasiri aliyefuata njia iliyonyooka. Hakukubali kununuliwa; alisimama, hata kama mwisho ulikuwa mbaya”, anasema Wagenknecht (mgombea kutoka Dietmar Bartsch). Ni mwanzilishi wa jumuiya ya wanamapinduzi wa Kisoshalisti, baadae chama cha Kikomunisti, cha Luxemburg, kwenye picha hii ya mwaka 1914, aliunga mkono tabaka la wafanyakazi.
Christian Lindner (FDP): Hans-Dietrich Genscher
""Genscher ni mongoni mwa watu mashuhuri katika taifa letu. Alikuwa kinara wa chama cha FDP” anasema Lindner aliyepiga picha na Genscher anayeonekana nyuma yake. Kwa takriban miaka 20, "waziri huyo wa mambo ya kigeni” aliitengeneza taswira ya Ujerumani nje, akijikita kwenye usalimishaji wa silaha na maridhiano na Mashariki. Kazi yake ya maisha ilihitimishwa na muungano wa Ujerumani mwaka 1990.
Alexander Gauland (AfD): Charles-Maurice de Talleyrand-Perigord
"Mmoja wa watu wa mfano wa kihistoria ni waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Talleyrand" kutoka siku ya Napoleon anasema Gauland "Anawakilisha kanuni ya uerevu: "mara zote msaidie adui kulinda heshima yake, kwa sababu utamuhitaji." Mlodi huyo wa karne ya 18 alichukuliwa kama mtafuta maslahi aliyehudumia mabwana wengi: kanisa, mapinduzi ya Ufaransa, Napoleon na wiski aina ya Bourbons.