1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yafuzu kwa 16 bora

24 Juni 2021

Ujerumani imefuzu awamu ya 16 bora katika michuano ya Euro 2020 kwa kutoka sare ya 2-2 na Hungary. Hapo Jumatano Ujerumani iliiponea chupu chupu na kujihakikishia nafasi ya kuingia katika raundi ya mtoano ya 16 bora.

https://p.dw.com/p/3vUox
Deutschland München | UEFA EURO 2020 | Portugal vs Deutschland | Tor 1:3
Picha: Alexander Hassenstein/Getty Images

Ujerumani imefuzu awamu ya 16 bora katika michuano ya Euro 2020 kwa kutoka sare ya 2-2 na Hungary. Hapo Jumatano Ujerumani iliiponea chupu chupu na kujihakikishia nafasi ya kuingia katika raundi ya mtoano ya 16 bora.

Ujerumani itaelekea mjini London ambako watakabiliana na wapinzani wao wa jadi Uingereza katika uga wa Wembley siku ya Jumanne.

"Nadhani itakuwa onyesho kali na tutajiandaa vizuri, " alisema kocha Joachim Löw.

Kipindi cha kwaza

Fußball EM EURO 2021 | Deutschland v Ungarn
Picha: Lukas Barth/AP/picture alliance

Adam Szalai alifungua kizuizi kwa Hungary baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Roland Sallai. Ujerumani ilikuwa na nafasi mara mbili za kusawazisha lakini Hungary waliongoza mechi hio hadi kipindi cha mapumziko.

Kai Havertz katika kipindi cha pili dakika ya 66 aliisawazishia Ujerumani, lakini sekunde kadhaa mambo yalibadilika tena na mchezaji wa Hungury Andras Schafer aliongeza bao la pili.

Ujerumani ilicheza kufa kupona na baada ya kocha Joachim Löw kufanya mabadiliko kadhaa katika safu ya mashambulizi, kunako dakika ya 83 Leon Goretzka alipachika wavuni bao na kuisawazishia Ujerumani.

Ujerumani ilimaliza na alama nne, pointi moja nyuma ya washindi wa kundi F Ufaransa, ambayo pia ilitoka sare ya 2-2 na Ureno. Ureno imefuzu katika raundi ya 16 bora huku Hungury ikibaduliwa katika mashindano hayo.

Mechi zijazo za raundi ya mchujo

Italien Rom | UEFA Euro 2020 | Tor für Italien
Picha: Claudio Villa/Getty Images

Siku ya Jumamosi Wales itachuana na Denmark, na Italia baada ya kumaliza kundi A kwa jumla ya pointi 9 itachuana na Austria.

Uholanzi itashuka dimbani kupimana nguvu na Jamuhuri ya Czech huku mabingwa watetezi Ureno wakitarajia kucheza na Ubelgiji siku ya Jumapili.

Siku ya Jumatatu, Croatia itacheza na Uhispania na Ufaransa itachuana na Uswisi.

Ujerumani siku ya Jumanne itaelekea Wembley kucheza na Uingereza na mechi kati ya Sweden na Ukrain ikamilishe michuano ya raundi ya 16 bora.

 

dpa