1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Mashambulizi ya mtandao kutoka nje yameongezeka

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Mamlaka ya Ujerumani hii leo imeripoti ongezeko la asilimia 28 la mashambulizi ya mtandaoni kutoka kwa wahalifu wa kigeni katika mwaka wa 2023.

https://p.dw.com/p/4fo3U
Mifumo ya kompyuta na mtandao
Urusi na China ndiyo zimetajwa kuwa maeneo yanayoongoza kuishambulia kimtandao Ujerumani.Picha: Silas Stein/imago images

Kulingana na data hiyo mpya, mashambulizi ya mtandaoni yanatoka hasa Urusi na China.

Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kitaifa kuhusu uhalifu wa mtandao, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani,  Nancy Faeser amesema, ''kiwango cha kitisho mtandaoni kinasalia kuwa juu.''

Hili ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo mashambulizi ya mtandaoni yaliongezeka kwa asilimia nane.

Kuna wasiwasi mkubwa juu ya washukiwa wa udukuzi na majasusi wakati huu wa maandalizi ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya. Na chama cha sekta ya kidijitali cha Ujerumani, Bitkom kiliripoti kuongezeka maradufu kwa idadi ya mashambulizi ya mtandao kutoka Urusi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Uharibifu wa kiuchumi unaosababishwa na uhalifu wa mtandaoni huigharimu Ujerumani euro bilioni 148 bilioni kwa mwaka.