Ujerumani kupewa ulinzi zaidi Euro 2016 | Michezo | DW | 16.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ujerumani kupewa ulinzi zaidi Euro 2016

Maafisa wa kandanda Ujerumani , watafanya mapitio ya usalama katika michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa kufuatia mashambulizi hayo ya kigaidi mjini Paris

Rais mwingine wa muda wa shirikisho hilo la DFB rainer Koch ameliambia gazeti la Bild leo Jumatatu kwamba shirikisho hilo litatafakari hatua gani nyingine zichukuliwe.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kililazimika kulala uwanjani Stade de France kaskazini mwa Paris baada ya pambano lao la kirafiki dhidi ya Ufaransa siku ya Ijumaa.

Mashambulizi hatari mjini Paris hayatadhuru nafasi za mji huo kuwa mwenyeji wa michezo ya majira ya joto ya Olimpiki mwaka 2024, amesema rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC Thomas Bach leo.

Mji ambao utakuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka 2024, utajulikana mwaka 2017 lakini Bach anaamini mashambulio mjini Paris , mji ambao umetangazwa kuwa moja na miji inayowania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, hayatakuwa na mwelekeo wowote katika matokeo ya kura itakayopigwa na kamati hiyo ya olimpiki.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com