1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kulegeza vikwazo vya kuzuia maambukizi ya corona

16 Februari 2022

Wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani wanatarajiwa kufanya kikao na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kujadili mpango wa kulegeza vikwazo vya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/476BD
Erste Ministerpräsidentenkonferenz unter Olaf Scholz
Picha: Michael Kappeler/REUTERS

Inaarifiwa kwamba sehemu kubwa ya vikwazo vilivyowekwa vitaondolewa kufikia Machi 20 huku watu wakikubaliwa kukutana tena katika mikutano ya kibinafsi.

Inaripotiwa kwamba sheria inayowakubalia watu waliochanjwa tu kuingia katika maduka na migahawa itaondolewa, ila uvaaji wa barakoa utasalia. Haya ni baada ya maambukizi ya virusi vya corona kupungua kwa siku kadhaa sasa Ujerumani.

Kwengineko New Zealand ambayo hadi mwezi Agosti mwaka jana ilikuwa haina maambukizi mapya, imerekodi maambukizi mapya leo (16.02.2022)

Haya yanafanyika wakati ambapo kuna maandamano ya kupinga vikwazo vilivyowekwa kuzuia maambukizi. Wizara ya afya nchini humo imeripoti visa 1,160 vya maambukizi mapya. 

Chanzo: afp