Uhariri : kuachiwa huru wakorea kusini waliotekwa nyara Afghanistan | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uhariri : kuachiwa huru wakorea kusini waliotekwa nyara Afghanistan

Wakati Wataliban wakijitayarisha kuwaachia huru mateka wao 7 waliobakia kutokana na wakorea kusini 23 waliowateka nyara wiki sita zilizopita, mkasa huu umegeuka kuwa wa aina yake katika matukio ya utekaji nyara. Baada ya kuwauwa mateka wawili hapo awali na kuwaachia wawili baadae, jana waliachiwa huru wengine 12,kutokana na majadiliano ya moja kwa moja na serikali ya Korea kusini.

Ni swala la wakati tu hadi pale mateka hao wa Kikorea kusini wataakapoungana tena na familia zao wakikumbatiana katika hali ya kwamba ni waliobahatika ,wakiwa mbele ya kamera za televisheni . Akina mama, Kina baba , watoto na kadhalika.-wote wana haki ya kufurahia kurudi nyumbani kwa jamaa zao.

Kutokana na kumalizika kwa mkasa huu wa utekaji nyara nchini Aghanistan kumetokeza pia ishara zenye athari: Kwa mara ya kwanza maafisa wa serikali wamejadiliana moja kwa moja na magaidi, jambo ambalo hadi sasa lilikua mwiko. Pili, kwa kufikia makubaliano na Watalibani na Korea kusini kuhidi kuyaondoa majeshi yake katika muda uliopangwa,hali hiyo imewapa uwanja wa propaganda Kwa hilo serikali ya Afghanistan inayoungwa mkono kimataifa na iliochaguliwa kidemokrasia imenufaika na nini ? Haikunufaika kabisa.

Samba na hayo hakuna tena kutumwa wamisionari wa kikristo Afghanistan , wala jumuiya ya kikristo zilizoko Hindukusch kuendelea kutoa misaada yao. Jengine lisiloelezeka linalotokana na tukio hilo na ni kuwa utekaji nyarav huu ni wa aina yake na wa ukatili wa kutosha. Ama kibaya zaidi ni kwamba hayo hayatokei tu nchini Afghanistan, bali pia Irak. Huko utekaji nyara kwa malengo ya kisiasa ni sawa na tukio la kila siku na dai la kutaka majeshi ya kigeni kuihama Irak au Afghanistan.

Kumalizika kwa kadhia hiyo ya mateka kunatoa ishara kwamba mikasa mengine ya aina hiyo itamalizikia hivyo hivyo. Swali la kwamba hakutatokea umwagaji damu au la, linabakia kuwa la kutabiri tu.

Nchi ya kwaaba kukumbwa na athari za hatua ya serikaliKorea kusini ni Ujerumani. Janga la kutekwa nyara bado linamkumba mhandisi wa kijerumani Rudolf Blechschmidt ambaye kwa majuma kadhaa sasa anashikiliwa huko Afghanistan. Tangu jana kiwango cha fidia aweze kuachiliwa huru kimeongezeka.

Kwa Wakorea kusini awawili miongoni mwa 23 waliotekwa nyara, kumalizika kwa mkasa huo kulichelewa kwani walipigwa risasi na kuuwawa. Bila shaka swali linaloulizwa ni jee jinsi mkasa huu ulivyoatatuliwa ni sawa ? Wanaosema ndiyo watakua wanawapigia magoti watekaji nyara- lakini pamoja na hayo kulikuweko na njia nyengine ?

Tangu Alhamisi inabakia wazi kwamba kuwakomboa waliotekwa nyara ni kazi ngumu. Ni Pigo kubwa,si kwa serikali tu bali hata yale mashirika ya misaada yanayosaidia katika ujenzi mpya wa Afghanistan.

 • Tarehe 30.08.2007
 • Mwandishi Mohammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH8m
 • Tarehe 30.08.2007
 • Mwandishi Mohammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH8m

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com