Uharamia bahari ya hindi wapamba moto | Habari za Ulimwengu | DW | 26.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Uharamia bahari ya hindi wapamba moto

Meli moja ya Ujerumani inayosafiri katika bahari ya hindi imelizima shambulio la silaha la maharamia wa Kisomali. Maafisa wa usalama ndani ya Meli hiyo MS Melody walijibu hujuma ya maharamia sita waliokua na bunduki wakati walipoikaribia wakiwa ndani ya mashua ya mwendo wa kasi.Maafisa wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ujerumani mjini Berlin hawakuweza kuthibitisha ripoti hizo, lakini wamesema unafanyika uchunguzi juu ya mkasa huo.

Hapo mapema maharamia wa Kisomali waliiteka nyara meli moja ya Ujerumani ikiwa na shehena ya tani 31.000 za nafaka katika ghuba ya Aden.

Afisa wa safari za meli nchini Kenya amesema meli hiyo ilitekwa nyara alfajiri na mabaharia wote 17 wako salama. Utekaji nyara katika pwani ya mashariki mwa Afrika umepamba moto mnamo wiki za karibuni, licha ya kuwepo kwa manuwari za kijeshi za nchi kadhaa za kigeni katika eneo hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com