1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

Ugumu wa maisha ajenda muhimu uchaguzi Bunge la Ulaya

John Juma
9 Mei 2024

Hali ngumu ya uchumi ni suala linalowagusa wengi ndani ya Umoja wa Ulaya. Je ni vipi unaweza kushawishi uchaguzi wa bunge la Ulaya?

https://p.dw.com/p/4ffxw
Uchaguzi wa Bunge la Ulaya kufanyika Juji 6 hadi 9.
Uchaguzi wa Bunge la Ulaya kufanyika Juji 6 hadi 9.Picha: Jean-Francois Badias/AP Photo/picture alliance

Mamilioni ya raia wa Umoja wa Ulaya wanaotarajiwa kupiga kura kati ya Juni 6 - 9, kuwachagua wajumbe 720 wa Bunge la umoja huo wanaghadhabishwa na hali ngumu ya maisha, inayowakabili kila kukicha.

Hali inayoweza kuathiri vyama vikuu kwenye uchaguzi wa chombo hicho muhimu katika kutunga sera za masuala mbalimbali ikiwemo biashara katika umoja huo wenye nchi 27.

Tangu uchaguzi uliopita mwaka 2019, Uchumi wa Ulaya umepata mapigo ikiwemo kufungwa kwa biashara wakati wa janga la COVID-19, kupanda kwa bei ya bidhaa kote ulimwenguni na hata kuathiriwa zaidi na bei ya juu ya nishati iliyochochewa na uvamizi wa Urusi ndani ya Ukraine.

Matukio ya kushambuliwa wanasiasa nchini Ujerumani kuelekea uchaguzi wa bunge la Ulaya, yaibuwa mshtuko.

Usaidizi mkubwa wa serikali kwa familia na biashara uliisaidia kuepusha mdororo mkubwa wa Uchumi. Lakini kama tu ilivyo Marekani ambapo juhudi hizo hazionekani kumsaidia sana Rais Joe Biden kwenye kampeni zake kuwania muhula mwingine wa urais Marekani, huenda usiwe chachu ya kutosha kwa viongozi wa Ulaya kuutumia kushawishi uungwaji mkono.

Ustahimilivu dhidi ya mapigo ya kiuchumi

Jeromin Zettelmeyer, mkurugenzi wa taasisi ya kiuchumi Bruegel iliyoko Brussels Ubelgiji, amesema inashangaza jinsi Ulaya imeweza kustahimili mapigo hayo, lakini ustahimilivu huo si jambo linaloleta matumaini makubwa.

Wachambuzi wanahoji, huenda raia wangependa viongozi wao kuyapa masuala ya ndani Wachambuzi wanahoji, kuwa hali ngumu ya maisha inawapa nguvu baadhi ya wanasiasa wenye misimamo mikali ya mirengo ya kulia.
Wachambuzi wanahoji, kuwa hali ngumu ya maisha inawapa nguvu baadhi ya wanasiasa wenye misimamo mikali ya mirengo ya kulia.Picha: LUDOVIC MARIN/AFP/Getty Images

Ameongeza kuwa wakati mwingine unahitaji kuanza kufikiria raia wa nchi yako kwanza, kabla ya wengine.

Kwa mfano rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anapaswa kuyapa kipaumbele masuala ya Wafaransa kama nyumba za bei nafuu, badala ya kufuatilia msaada kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Kitisho cha ongezeko la Umaskini

Kwa sasa, vyama vikuu, ambavyo vina ushawishi mkubwa katika Bunge la Ulaya na vilevile katika siasa za ndani ya nchi zao, vina karibu mitazamo inayofanana ya kuwa na biashara ya wazi na mataifa mengine ulimwenguni.

Chama cha Le Pen chazindua kampeni uchaguzi wa Bunge la Ulaya

Lakini makubaliano hayo yako hatarini kwani raia wengi wa Ulaya wanaungana kwa kauli moja kwamba hali ya uchumi iliyopo haifanyi kazi kwao.

Mwaka uliopita pato la Ulaya likikua kwa asilimia 0.5, huku ukosefu ajira ukiwa asilimia 6.5 hiyo ikiwa chini kuwahi shuhudiwa katika historia yake.

Lakini tathmini ya ndani ya takwimu hizo zinakuacha na mshangao wa jinsi mamilioni ya raia wa Ulaya wakiwemo wanaofanya kazi wanatatizika na upungufu wa fedha kuyakidhi mahitaji yao.

Uchaguzi wa Bunge la Ulaya 2024 | Bunge la Ulaya kule Straßburg 2023
​​​​​​Kulingana na wachambuzi, masuala mengi ikiwemo siasa na miungano itakayoundwa kuelekea uchaguzi huo yatakuwa na ushawishi kwenye debe.Picha: Daniel Kalker/picture alliance

Kulingana na utafiti wa kila mwaka wa taasisi ya R+V ya Ujerumani, masuala matatu makubwa kwa Wajerumani yamefungamana na fedha, ikiwemo  gharama ya juu ya maisha, kodi ya juu ya nyumba na hofu ya kupunguzwa kwa ruzuku au michango ya serikali.

Hofu  ya raia kutoweza kuyakidhi mahitaji yao

Isabelle Borucki, profesa katika chuo kikuu cha Philipps Maarbug Ujerumani amesema, raia wanahofu ikiwa wataweza kuyakidhi mahitaji yao kifedha.

Hofu kama hiyo pia inashuhudiwa Uhispania, Poland na kwingineko ambako viwango vya riba kwa wamiliki majumba vimeongezeka.

AfD kuamua wagombea wake katika bunge la Ulaya

Jinsi masuala hayo yote yatakavyoathiri bunge la nchi 27 wanachama, hakika itategemea masuala mengine ikiwemo siasa na miungano itakayoundwa kuelekea uchaguzi huo.

Kura za maoni zinaonesha vyama vikubwa vya mirengo ya kulia na shoto vikiongoza katika nchi 16. Lakini pia zinaonesha makundi yenye misimamo mikali yakijiongezea ushawishi kuwa na uwezo wa kushinda moja juu ya tano ya viti vya bunge la Ulaya. Na hali ya watu kutoridhishwa na hatua za kiuchumi huenda inachangia hayo.

(Chanzo: RTRE)