1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

Bei ya mafuta yapungua kwa dola 1 kwa pipa

6 Machi 2026

Bei ya mafuta imepungua kwa angalau dola moja kwa pipa kwenye soko la dunia leo Ijumaa baada ya Marekani kutangaza kulegeza vikwazo na kuipatia ruhusa India kununua shehena ya mafuta kutoka Urusi.

https://p.dw.com/p/59uaY
Kuwait Mina Al Ahmadi 2008 | Meli ya mafuta ikipakia shehena kwenye bandari ya Hafen Mina Al Ahmadi
Vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Israel vimeyumbisha usambazaji mafuta duniani. Picha: Gustavo Ferrari/AP Photo/picture alliance

Taarifa za masoko zinaonesha pipa moja la mafuta ghafi sasa linauzwa kwa dola 84.8 za kimarekani kutoka dola 85.1 jana Alhamisi.

Bei hiyo ni pungufu ya karibu dola moja tangu gharama za nishati ya mafuta zilipopanda kwa kasi duniani baada ya Marekani na Israel kuishambulia Iran jumamosi iliyopita.

Katika kupunguza msukosuko Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent amesema wameondoa zuio kwa siku 30 na kuiruhusu India kununua mafuta ya Urusi yaliyokwama baharini.

Hatua hiyo imechukuliwa katika wakati usafirishaji mafuta kupitia ujia muhimu wa mlango bahari wa Hormuz umeporomoka kwa asilimia 90 kutokana na mapigamo yanayoendelea.