Tuzo ya mashika ya wachapisha vitabu ya Ujerumani atunukiwa Friedländer
14 Oktoba 2007Matangazo
Frankfurt Am Main:
Mtaalam wa Taareh wa Israel,Saul Friedländer ametunukiwa hii leo zawadi ya amani ya shirika la wachapisha vitabu nchini Ujerumani.Mtaalam huyo wa historia mwenye umri wa miaka 75 amekabidhiwa tuzo hiyo yenye thamani ya yuro 25 elfu katika kanisa la Paul mjini Frankfurt.Friedländer anaeishi nchini Marekani,amepata umashuhuri mkubwa kutokana na kitabu chake „Enzi ya tatu na wayahudi“ akichambua mauwaji ya halaiki ya wayahudi yaliyofanywa na wanazi katika vita vikuu vya pili vya dunia Holaucust