1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Mazungumzo ya kibiashara yalikuwa mazuri

11 Oktoba 2019

Mazungumzo muhimu ya kibiashara kati ya China na Marekani yanaingia siku ya pili leo Ijumaa huku kukiwa na hali ya matumaini baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema majadiliano ya siku ya kwanza yalikuwa mazuri. 

https://p.dw.com/p/3R73j
USA Trump zu Ukraine-Affäre und China
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Getty Images/AFP/J. Watson

Rais Trump amesema atawakaribisha leo katika Ikulu ya white house wajumbe wanaoshirikia mazungumzo hayo akiwemo Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He anayeongeza ujumbe wa nchi yake kwenye awamu hiyo ya 13 ya mazungumzo magumu ya biashara.

Ujumbe wa Marekani unaongozwa na waziri wa fedha  Steven Mnuchin na mwakilishi wa biashara wa Marekani Robert Lighthizer na pande zote mbili zimeyaelezea mazungumzo hayo kuwa ishara ya nia njema.

Matarajio yalikuwa madogo kwamba majadiliano hayo hayatofanikiwa kutoa na majibu ya msingi katika kutatua vita vya kibishara vya miezi 15 baina ya mataifa hayo yenye duniani.

Mataifa hayo yamo kwenye mkwamo juu ya madai ya Marekani kwamba China inaiba teknolojia pamoja ya kuyalazimisha mapakampuni ya nje kutoa siri za kibiashara kama sehemu ya kampeni yake ya kuwa taifa kiongozi kwenye sekta ya viwanda hasa vya maroboti na magari.

Ishara za kurejea utulivu kati ya Washington na Beijing

USA und China verhandeln neues Handelsabkommen
Wajumbe wa Marekani na China katika mazungumzo ya biasharaPicha: picture-alliance/Xinhua/L. Jie

Matamshi ya Trump ya kusifu mazungumzo ya siku ya kwanza yameashiria kurejea kwa hali ya utulivu kati ya pande mbili ambazo wiki moja iliyopita zilikuwa kwenye kiwango cha juu cha uhasama.

Marekani iliidhibu China kwa hatua kali za kisera na zilisalia siku chache kabla ya kutekelezwa kwa nyongeza ya ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 250.

Ikulu ya Marekani imesema mada muhimu kwenye awamu hii ya mazungumzo ni pamoja na uhamishaji wa lazima wa teknolojia, hakimiliki za ubunifu, vikwazo visivyo vya kikodi na sekta ya kilimo.

Idara ya biashara ya taifa nchini Marekani imedokeza kuwa wajumbe wa majadiliano wanaweza kufikia makubaliano katika masuala ya ulinzi wa sarafu na hakimiliki ambayo huenda yakasitisha nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za China iliyopangwa kutekekelezwa Oktoba 15.

China iko tayari kutoa suluhisho

NBA China Games 2019 | Los Angeles Lakers vs Brooklyn Nets
Picha: Getty Images/L. Zhang

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa China inajitayarisha kutoa mapendekezo ambayo hayatoshughulikia pakubwa malalamiko ya rais Trump lakini yataongeza manunuzi ya bidhaa za kilimo za Marekani kwa matumaini ya kusitishwa nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za China.

Alipoulizwa na waandishi habari juu ya iwapo yuko tayari kuridhika na hata makubaliano madogo yatakayofikiwa kwenye mazungumzo hayo, rais Trump alijizuia kusema chochote.

Masoko ya mitaji nchini Marekani ikiwemo Wall Street yameimarika kuufutia matamshi ya mataumaini huku wengi wakitarajia uwezekano wa kufikiwa makubaliano au kusitishwa kwa vita vya kibiashara.

Katika wiki za karibuni shinikizo limeongezeka kati ya pande hizo mbili la kuzitaka kupunguza makabilinao baada ya ishara zote kuonesha vita vya kiabsra kati ya Marekani na China vinatoa kitisho kikubwa kwa uchumi wa ulimwengu.