Trump atishia kuwapeleka maafisa wa ICE viwanja vya ndege
23 Machi 2026
Siku ya Jumamosi Trump alitishia kuwapeleka maafisa wa ICE kwenye viwanja vya ndege Jumatatu ikiwa wabunge wa Democratic hawatakubali mara moja kufadhili shughuli za usalama wa viwanja vya ndege. Kufungwa kwa shughuli hizo ni matokeo ya mzozo kuhusu ufadhili wa Wizara ya Usalama wa Ndani, ambayo ndio shirika inasimamia idara za TSA na ICE. Maafisa wa ICE hawajafunzwa mahususi kwa ajili ya usalama wa viwanja vya ndege, ambao hufanywa na idara ya TSA.
Idara ya Usalama wa Uchukuzi ina wafanyakazi 65,000, wakiwemo maafisa 50,000 wa usalama wa viwanja vya ndege. Idara ya Uhamiaji na Forodha imekuwa na jukumu muhimu katika msako mkali wa uhamiaji unaofanywa na utawala wa Trump. Ukandamizaji huo wenye utata unakosolewa na Wademokrat wengi, watetezi wa haki za kiraia na makundi ya utetezi wa sera za uhamiaji.