1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi Mexico lawauwa watu 12 wenye silaha karibu na Marekani

19 Februari 2024

Wanajeshi wa Mexico waliokuwa wakifanya doria wamewauwa watu 12 wenye silaha kufuatia mapigano yaliyozuka eneo la Tamaulipas, ambalo limekumbwa na ghasia zinazohusishwa na magenge na walanguzi wa madawa ya kulevya.

https://p.dw.com/p/4caO0
Polisi Mexico katika oparesheni maalum ya kukabiliana na magenge ya uhalifu
Polisi Mexico katika oparesheni maalum ya kukabiliana na magenge ya uhalifuPicha: Francisco Robles/AFP/Getty Images

Mamlaka za usalama eneo hilo zimeeleza kuwa majibizano ya risasi yalitokea katika manispaa ya Miguel Aleman kwenye mpaka na Marekani baada ya maafisa kushambuliwa na watu wenye silaha waliokuwa wamejificha msituni. Jeshi la Mexico lilitumia droni na helikopta katika operesheni hiyo.

Soma pia:Watu wapatao 10 wauwawa Ecuador

Tangu kuanzishwa  kwa operesheni kabambe ya kijeshi ya kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya mnamo mwaka 2006,  Mexico imeshuhudia visa 420,000 vya mauaji huku karibu watu 110,000 wakitoweka. Idadi kubwa ya matukio hayo yanahusishwa na magenge ya uhalifu.