1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump atishia kuiondoa Marekani katika muungano wa NATO

1 Aprili 2026

Mvutano kati ya Marekani na washirika wake wa Jumuiya ya Kujihami NATO umeongezeka, baada ya Rais Donald Trump kusema anafikiria kuiondoa nchi yake kwenye muungano huo wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/5BWqg
USA West Palm Beach 2026 | Donald Trump steigt in die Air Force One
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/dpa/picture alliance

Trump amesema baadhi ya wanachama wa Jumuiya hiyo wamekataa kutuma meli zao za kivita kusaidia kuufungua Mlango Bahari wa Hormuz.

NATO, inayojumuisha nchi za Ulaya, Marekani na Canada, iliundwa mwaka 1949 kwa lengo la kukabiliana na tishio la mashambulizi ya Umoja wa Kisovieti na kwa miongo kadhaa imekuwa nguzo muhimu ya usalama wa nchi za Magharibi.

Kauli ya Trump imejiri saa chache baada ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, kushindwa kuhakikisha dhamira ya Marekani katika ulinzi wa pamoja wa NATO, hakikisho ambalo ni muhimu kwa muungano huo.

Kwa muda mrefu wataalamu wamekuwa wakionya kuwa kauli zinazoonesha kwamba haiko tayari kuwa pamoja na NATO na kuifanya Urusi kuendelea kuwa kitisho kwa Ulaya.